Opresheni kubwaa ya kupuliza dawa kwenye maeneo ya Aizidiyyina katika mji wa Mosul

Maoni katika picha
Miongoni mwa opresheni zilizo ratibiwa na idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maeneo wanayo ishi jamii ya Aizidiyyina katika mkoa wa Mosul, ni opresheni kubwa ya kupuliza dawa iliyo fanywa na kamati ya kupambana na maambukizi chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau/26 Hashdu-Shaábi.

Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati hiyo Ali Abdurahim Ahmadi amesema: “Hakika kazi hii ni sehemu ya kazi nyingi zinazo fanywa na kamati yetu tangu yalipoanza maambukizi ya virusi vya Korona, tumesha puliza kwenye mikoa mingi na bado tunaendelea, leo tunaendelea kutekeleza wajibu wa kibinaadamu wa kupuliza dawa kwenye maeneo kadhaa wanayo ishi Aizidiyyina, chini ya idara ya ustawi wa jamii, vifaa vya kisasa vinatumika katika opresheni hiyo, pamoja na gari maalum ambapo lita (6000) za dawa zitatumika katika opresheni hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Opresheni hii inahusisha jengo la Narjisi wanapo ishi wakimbizi wa kabila la Aizidiyyina katika kijiji kilichopo wilaya ya Sanjaar pamoja na maeneo ya wilaya ya Sanjaar na Maqaam ya bibi Zainabu (a.s) na Bartwala, Bahzani na Baáshiqah”.

Wakazi wa vitongoji hivyo wametoa shukrani za dhati kwa watendaji wa opresheni hii inayo dhihirisha mapenzi makubwa na uzalendo wa kweli, kwani wamekuja haraka kupuliza dawa baada ya kuripotiwa kisa cha maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa kikosi kilikua kimesha unda kamati ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona tangu maambukizi ya virusi hivyo yalipo anza kuripotiwa, na wamesha puliza dawa sehemu nyingi za makazi ya watu, ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na wanatumia uwezo wote katika kufanikisha kazi hiyo, aidha wamejenga kituo maalum cha kuosha, kuvisha sanda na kuzika watu waliokufa kwa ugonjwa wa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: