Makumbusho ya Alkafeel imetoa wito wa kushiriki katika kongamano la kimataifa awamu ya tatu

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel la kimataifa awamu ya tatu imetoa wito kwa watafiti na wasomi wa kushiriki kwenye kongamano la kimataifa awamu ya tatu, litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Makumbusho na vifaa vya kisasa), siku ya Jumamosi mwezi (5 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (21 Novemba 2020m) kupitia jukwaa la (ZOOM).

Rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Swadiq Laazim amesema kuwa: “Kongamano hili liliahirishwa na kusogezwa mbele kutokana na janga la Korona, sasa litafanywa kwa njia ya mtandao badala ya watu kuja, kutokana na mazingira ya sasa kamati imelazimika kuendesha kongamano hilo kwa njia ya mtandao na mada zitakazo wasilishwa ni zilezile, ambazo ni:

  • - Mbinu za kutunza taarifa za makumbusho.
  • - Makumbusho katika mitandao ya kielimu na mawasiliano ya kijamii.
  • - Teknolojia za kisasa katika maonyesho ya makumbusho.
  • - Elimu na teknolojia za kisasa katika kutunza majengo ya makumbusho.
  • - Teknolojia za kielimu na njia za kisasa katika kusanifu makumbusho zinazo tembelewa kwa njia ya mtandao.
  • - Kuongeza uwezo wa kuongoza makumbusho”.

Akafafanua kuwa: “Link ya kushiriki kwenye kongamano hilo ni: https://zoom.us/j/93275677716?pwd=QnZUa2VpNzBTSEV1WHZYVnVpUStRUT09
namba ya kuingia kwenye kikao ni (7716 7567 932) kutakua na vikao vitatu ambavyo mada za kitafiti zitawasilishwa na wasomi kutoka ndani na nje ya Iraq, tunatarajia awamu hii itakua muendelezo wa mafanikio ya awamu zilizo tangulia”.

Kumbuka kuwa kongamano linalenga mambo yafuatayo:

  • - Wito wa kutunza turathi na tamaduni.
  • - Kusaidia taasisi za Dini na za kiraia kuanzisha makumbusho na kuendeleza kazi za makumbusho.
  • - Kufungua uwanja wa kushirikiana na taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa na kuziendeleza.
  • - Kuboresha utendaji wa kazi za makumbusho kiidara na kivifaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: