Atabatu Abbasiyya tukufu na serikali ya mkoa wa Karbala wamefanya usanifu wa mwisho wa upanuzi wa eneo la mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad)

Maoni katika picha
Jioni ya siku ya Jumanne (1 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (17 Novemba 2020m) kimefanyika kikao kilicho husisha katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu pamoja na rais wa kitengo cha kihandisi, na mkurugenzi wa mkoa wa Karbala na msaidizi wake na baadhi ya wahandisi bila kumsahau mkuu wa kikosi cha kulinda haram mbili tukufu na kikundi cha wataalam wa mkoa wa Karbala.

Kikao hicho kimefavya ndani ya Ataba tukufu kwa ajili ya kuwasilisha usanifu wa mwisho wa upanuzi wa mlango wa mji mkongwe upande wa mashariki (eneo la Baabu Bagdad).

Kumbuka kuwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi, walitembelea eneo la mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad) linalo elekea katika malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuweka mkakati wa kupanua eneo hilo, na kulifanya liendane na wingi wa mazuwaru wanaopita hapo hususan katika ziara zinazo hudhuruwa na mamilioni ya watu.

Ziara hiyo ilihusisha wajumbe kadhaa wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wataalamu, bila kusahau wawakilishi wa serikali ya Karbala na ofisi ya wataalam kutoka chuo kikuu cha Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: