Kwa ajili ya kuongeza kiwango cha uwajibikaji: Kitengo cha malezi na elimu ya juu kimemaliza mafunzo ya kujenga uwezo

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza mafunzo mapya yaliyo tolewa kwa walimu wa michezo ya watoto, hii inatokana na Atabatu Abbasiyya tukufu kutilia umuhimu swala hilo, kupitia watumishi wake wanaofanya kazi kwenye sekta tofauti, hususan sekta ya elimu kutokana na umuhimu wake.

Shule za Al-Ameed zinafanya vizuri katika michezo, na zinamikakati ya kuongeza kiwango chao hususan kwenye michezo ya watoto, kwa kutoa mafunzo mbalimbali, Dokta Ahmadi Swabihu Kaábi rais wa kitengo hicho ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunafundisha michezo tofauti kwa kufuata ratiba maalum ya malezi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kutoa semina kwa walimu na kuwafanya waendane na maendeleo yanayo tokea kwenye sekta ya michezo duniani”.

Akaongeza kuwa: “Mafunzo mapya yametolewa rasmi kwa walimu wa michezo ya watoto, wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo, mafunzo hayo yamehitimishwa hivi karibuni baada ya kufikiwa malengo yaliyo kusudiwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: