Mabalozi wa utamaduni wa nchi: Stempu za barua zinawakilisha visa vya jamii katika makumbusho ya vifaa na nakala-kale Alkafeel

Maoni katika picha
Makumbusho ya vifaa na nakala-kale Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa vitu vilivyopo katika makumbusho hiyo ni stempu za barua zilizo kuwa zikitumika hapa nchini na katika nchi zingine, sehemu hiyo imeongezwa hivi karibuni katika makumbusho hiyo, inatokana na mkakati wa kuifanya kuwa makumbusho ya kila kitu, na sehemu ya vitu muhimu katika historia ni stempu za barua, kwani zinabeba ujumbe mkubwa wa kijamii, ni balozi anayehamisha utamaduni, ramani na mila za taifa katika historia.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim Zaidi, amesema kuwa: “Kukusanya stempu za barua ni moja ya mbinu za kuboresha makumbusho, tumeanza kufanya hivyo muda mrefu, baada ya kutembelea makumbusho zingine za kitaifa na kimataifa, tulizikuta zina sehemu maalum ya stempu, tukaona na sisi tufanye hivyo, hadi sasa tumesha kusanya jumla ya stempu (11,493) kutoka nchi (128) za kiarabu na kiajemi bila kuisahau Iraq”.

Akabainisha kuwa: “Stempu zimewekwa kwa kufuata utaratibu wa miaka na herufi pamoja na nchi husika, na bendera yake na tukio la kutengenezwa kwake, kila stempu inawekwa pamoja na maelezo yake, kila albamu ina namba zinazo iwezesha kutambulika kwa urahisi”.

Akafafanua kuwa: “Pamoja na hayo tumetengeneza program ya kielektronik kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusu stempu hizo, sambamba na kuweka mtaalamu aliyebobea katika kuhifadhi mambo kiteknolojia, baada ya kupewa semina maalum ya kazi hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: