Maoni katika picha
Msaidizi wa mkuu wa chuo katika mambo ya kiidara Dokta Alaa Mussawi amesema kuwa: “Hakika hafla hii inayofanywa na uongozi wa kitivo, inalenga kutoa zawadi kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri mwaka jana pamoja na changamoto zilizo kuwepo”.
Akaongeza kuwa: “Tunaona fahari kuwa na kitivo cha famasiya cha aina hii, ambacho uzuri wake umeonekana wazi kwa wanafunzi wake katika mwaka wa kwanza”.
Naye mkuu wa kitivo cha famasiya katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Ahmadi Hashim Rifai amesema: “Kutokana na msingi wa kukamilishana na kuendelezana leo tunafanya mahafali ya kumaliza mwaka wa kwanza toka kuanzishwa kitivo hiki, pamoja na kuwa na umri mdogo lakini kinamafanikio makubwa ya kujivunia kushinda hata baadhi ya vyuo vikuu vikongwe”.
Akasisitiza kuwa: “Mafanikio hayo yasingepatikana kama sio msaada endelevu wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na uwajibikaji wa moja kwa moja wa rais wa chuo”.