Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea mkoa wa Waasit na kukutana na viongozi wa makabila na watu maarufu, chini ya ratiba ya mawasiliano iliyo andaliwa na Ataba tukufu kwa lengo hilo, na ambayo inalenga kuongeza mawasiliano na jamii.
Ujumbe huo umeongozwa na Sayyid Adnani Mussawi kutoka kitengo cha Dini katika Ataba tukufu, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ziara hii ni sehemu ya ratiba ya kuwasiliana na raia wa Iraq na watu wa tabaka tofauti, kuja kwetu katika mkoa huu mtukufu kwanza ni kwa ajili ya kutoa pole kwa kuondokewa na kiongozi wa kabila la Saari Shekh Khayuni hapa Iraq na nchi za kiarabu, aliyekufa kwa maradhi ya Korona, tumepokelewa na kiongozi aliyechukua nafasi yake Shekh Khalidi Atwaar Faalih Kaswabi, ambaye tumemfikishia salamu na pole kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na dua yake kwa marehem ya kumtakia magharifa na shifaa kwa maimamu watakasifu (a.s), ndugu wa marehemu wameshukuru sana kupata salamu hizo na wakaomba uongozi wa Ataba uendelee kuwa na amani na kuhifadhika”.
Akaendelea kusema: “Hali kadhalika tulitembelea ofisi ya marehemu Sayyid Abdul-Adhim Yaasiri na tukakutana na Sayyid Kaamil Abdu-Adhim Yaasiri, halafu tukatembelea sehemu ya familia ya Zirkani katika mkoa wa Waasit, ambapo tumekutana na kundi la viongozi na tukazungumza mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuongeza ushirikiano na ulazima wa kushikamana na misingi ya sheria kuhusu maswala ya fidia kama yanavyo elekezwa na Dini tukufu ndani ya Quráni na sunna za Mtume (s.a.w.w), tukamtembelea pia majeruhi wa Hashdu-Shaábi na kuwatakia afya njema”.
Mwisho wa ziara hiyo ambayo tulifuatana na Mu’tamad Marjaiyya Mheshimiwa Shekh Mujahidi Muhammad Zarkani, tukatembelea malalo ya Swahaba mtukufu Saidi bun Jubair (r.a) katika wilaya ya Hai.