Wanafunzi 45 wa kiume na wa kike kutoka kwenye shule za Al-Ameed wamepata nafasi katika shule za wanafunzi wenye vipaji maalum

Maoni katika picha
Wanafunzi 45 wa kiume na wa kike kutoka kwenye shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamepata nafasi katika shule za vipaji maalum mkoani Karbala, sawa na asilimia %25 ya wanafunzi waliochaguliwa kutoka mikoa yote ya Iraq.

Hivyo kitengo kimefanya halfa maalum ya kuwapongeza wanafunzi na walimu kwa mafanikio hayo, iliyo hudhuriwa na wanafunzi pamoja na wazazi wao na watumishi wa elimu.

Katika hafla hiyo rais wa kitengo Dokta Ahmadi Kaabi amesema kuwa: “Zawadi hizi ni sehemu ya kupongeza kazi nzuri inayofanywa na shule za Al-Ameed kuanzia shule zake za awali hadi darasa la sita shule ya msingi, ambapo wameweza kufaulu zizuri na kuchakuliwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule za wenye vipaji maalum”.

Akafafanua kuwa: “Miongoni mwa sifa nzuri za shule hizi, huendelea kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi hadi ngazi za juu, kwa hiyo wataendelea kuwasiliana na wanafunzi wake waliochaguliwa katika shule za vipaji maalum miaka yote, na kuhakikisha mbegu hii iliyoanza kutoa matunda pamoja na sisi itakamilisha safari yake hadi chuo Insha-Allah”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunawashukuru watu wote walio hudhuria hususan walimu na wazazi mliofanya kazi kubwa ya kusaidia vijana wenu kupata mafanikio haya, pamoja na kudumisha kwenu mawasiliano na uongozi wa shule katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi”.

Wazazi wameshukuru kufanywa hafla hii na wamepongeza kazi nzuri inayo fanywa na shule za Al-Ameed ambayo imeonyesha mafanikio haya makuba, na jinsi wanavyo lea akili za wanafunzi wao na kuwafanya kuwa mfano mwema na wa kuigwa katika sekta ya elimu na maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: