Makumbusho ya Alkafeel yatangaza ratiba ya kongamano la kimataifa awamu ya tatu

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa Alkafeel awamu ya tatu imetangaza ratiba ya kongamano litakalo anza Jumamosi asubuhi mwezi (5 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (21 Novemba 2020m) kupitia jukwaa la (ZOOM) chini ya kauli mbiu isemayo (Makumbusho na teknolojia za kisasa).

Rais wa makumbusho ya vifaa na nakala-kale Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi Ustadh Swadiq Laazim amesema kuwa: “Kongamano litanfanywa kwa kutumia ZOOM kupitia link ifuatayo: https://zoom.us/j/93275677716?pwd=QnZUa2VpNzBTSEV1WHZYVnVpUStRUT09

Litafunguliwa saa tatu asubuhi, namba za kuingia kwenye kikao ni (932 7567 7716), ratiba ya ufunguzi itakua kama ifuatavyo:

  • - Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Ujumbe kutoka kamati kuu ya athari na turathi.
  • - Ujumbe kutoka nchi za kiarabu.
  • - Filamu inayo onyesha harakati muhimu zinazo fanywa na makumbusho”.

Akafafanua kuwa: “Kutakuwa na vikao vitatu vya kuwasilisha mada za kitafiti, kikao cha asubuhi kitaanza saa nne, jumla ya mada tano zitawasilishwa, na kikao cha pili kitaanza saa tisa na dakika kumi, na kikao cha jioni kitakua na mada tatu, kitahitimishwa kwa kuweka maazimio ya kongamano na kugawa vyeti vya ushiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: