Kuanza vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti katika kongamano la kimataifa Alkafeel awamu ya tatu

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa wasomi wa mambo ya makumbusho kutoka ndani na nje ya Iraq, asubuhi ya Jumamosi (5 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (21 Novemba 2020m) kimefanyika kikao cha kwanza cha kongamano la kimataifa Alkafeel awamu ya tatu kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (ZOOM) chini ya kauli mbiu isemayo (Makumbusho na teknolojia za kisasa).

Kikoa hicho kimeongozwa na Dokta Muhammad Rukani kutoka chuo kikuu cha Qadisiyyah na Dokta Ahmadi Naji Sabí kutoka chuo kikuu cha Kufa, jumla ya mada tano zimewasilishwa kama ifuatavyo:

Mada ya kwanza: imetolewa na Dokta Yusufu Hajim Twaiy kutoka chuo kikuu cha Kufa, isemayo (Nafasi ya rasilimali watu katika ubunifu kwenye makumbusho ya Alkafeel).

Mada ya pili: imetolewa na Dokta Abbasi Mindili kutoka makumbusho ya Iraq, inasema (Misingi ya uongozi wa makumbusho na nafasi yake katika kulinda turathi na mazingira).

Mada ya tatu: imetolewa na Dokta Daliya Ali Abdul-Aadil Sayyid pamoja na Dokta Imani Muhammad Othumani na Dokta Yasini Sayyid Zidani kutoka makumbusho ya Misri, wamewasilisha utafiti na uzowefu wa kutumia mitambo ya kisasa katika kusafisha malikale.

Mada ya nne: imetolewa na Dokta Dhwargham Ali Muslim pamoja na Dokta Amiru Ni’mah Karbalai na Rafidu Hamidi Hadharawi kutoka chuo kikuu cha Kufa, isemayo (Wafanya kazi wa makumbusho na jinsi ya kuvutia wageni).

Mada ya tano: imetolewa na Dokta Dhiyaau Ni’mah Muhammad kutoka chuo kikuu cha Baabil, isemayo (Zana za kurekebisha nakala-kale zilizo haribika katika Atabatu Abbasiyya tukufu).

Kikao hicho kimeshuhudia maswali na maoni mengi kutoka kwa washiriki, watoa mada wamejibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.

Tambua kuwa hiki ni kikao cha kwanza katika kongamano lenye vikao vitatu, wameshiriki watafiti kutoka vyuo vikuu vya Iraq (Baabil, Kufa, Bagdad, Swalahu-Dini, Muthanna, Mustanswariyyah na Qadisiyya) na kutoka kwenye makumbusho za Iraq: (Makumbusho ya Qashlah, makumbusho ya Iraq, makumbusho ya kawaika katika mji wa Basra) na makumbusho ya Misri (makumbusho ya athari za turathi za Iraq, mada mbalimbali za kitafiti kuhusu makumbusho zitawasilishwa, zote zitahusu mambo mawili makubwa: kwanza ni kuhusu makumbusho na uboreshwaji wake pamoja na utumishi katika makumbusho sambamba na nafasi ya makumbusho katika kuchochea utamaduni na utalii, na nafasi ya rasili mali katika kuendeleza makumbusho na misingi ya uongozi wa makumbusho katika kulinda mazingira na mengineyo.

Sehemu ya pili, itakuwa na mada zinazo husu teknolojia ya kisasa katika kulinda misingi ya elimu na usanifu wa makumbusho, na njia za ukarabati wa vifaa na nakala-kale na utumiaji wa vifaa vya kisasa kwenye makumbusho na sehemu zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: