Kwa usomaji wa maazimio: Limehitimishwa kongamano la kimataifa la Alkafeel awamu ya tatu

Maoni katika picha
Jioni ya Jumamosi (5 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (21 Novemba 2020m) imehitimishwa awamu ya tatu ya kongamano la kimataifa kuhusu makumbusho Alkafeel lililo fanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (ZOOM) chini ya kauli mbiu isemayo (Makumbusho na teknolojia za kisasa), lililo simamiwa na makumbusho ya vifaa na nakala-kale Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kushiriki watafiti na wasomi kutoka vyuo vikuu vya Iraq: (Baabil, Kufa, Bagdad, Swalahu-Dini, Muthanna, Mustanswariyya na Qadisiyya), na kutoka katika makumbusho za Iraq (Makumbusho ya Qashlah, makumbusho ya Iraqiyya na makumbusho ya kawaida ya Basra), pamoja na athari na turathi za Iraq na (makumbusho ya Misri).

Katika ufungaji wa kongamano hilo rais wa kamati ya elimu Dokta Ibrahim Sarhani Shimri amesoma maazimio ya kongamano yafuatayo:

  • 1- Kongamano linaomba mambo yaliyo ibuliwa na watafiti kupitia mada zilizo wasilishwa yafanyiwe kazi, kutokana na umuhimu wake katika kuendeleza makumbusho na kutunza vitu vinavyo onyeshwa ndani ya makumbusho.
  • 2- Umuhimu wa kunufaika na elimu saidizi katika kutunza turathi baada ya utafiti kugundua njia tofauti za elimu kwa kutumia vifaa vya maabara na kemiya kutunza vitu na kutengeneza vilivyo haribika.
  • 3- Umuhimu wa kuendana na maendeleo ya dunia na kuweka misingi ya kushirikiana na vyuo vikuu vya kigeni pamoja na makumbusho, na kunufaika na uzowefu wao katika fani mpya za utunzaji kwa kutumia elimu za kisasa, na tunapongeza ushirikiano uliopo kati ya kitivo cha adabu katika chuo kikuu cha Bagdad na Ujerumani ambao umepelekea kuanzishwa shirika la kubadilishana uzowefu na kukuza uwezo wa watafiti na wanafunzi wa elimu ya juu na kufanya kazi kwa ushirikiano.
  • 4- Wanakongamano wanaomba vitengo vya athari (mambo-kale) katika vyuo vikuu vya Iraq viangalie upya mitaala yao ya elimu na iboreshwa sawa na maendeleo ya sasa katika sekta ya makumbusho, kwani mitaala iliyopo inaupungufu kutokana na ukongwe wake.
  • 5- Vyuo na vitengo vya athari (mambo-kale) vimetoa wito wa kunufaika na uzowefu wa makumbusho ya Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia namna inavyo onyesha na kutunza mali-kale zake, na wanafunzi wa elimu ya juu wanaombwa kufanya tafiti kupitia mali-kale zinazo milikiwa na Ataba tukufu.
  • 6- Wanakongamano wanaomba kuendelea kwa kongamano hili, kwa muda utakao pangwa na utaratibu ambao uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya utaona unafaa, na kudumisha mawasiliano na wadau wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: