Kitengo cha utumishi kinafanya opresheni ya usafi kwenye malango makuu ya kuingia Karbala

Maoni katika picha
Wafanyakazi wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya upresheni kubwa ya usafi, inahusisha malango makuu na barabara zinazo ingia katika mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kuhakikisha mji unakuwa na muonekano mzuri.

Tumeongea na makamo rais wa kitengo hicho bwana Muhammad Harbi kuhusu opresheni hiyo amesema kuwa: “Hii ni moja na kazi ambazo hufanywa na kitengo chetu katika kipindi chote cha mwaka, watumishi wetu wameanza kufanya usafi mapema leo asubuhi, kwa kuanzia barabara ya (Baabil – Karbala), baada ya hapo wataelekea katika maeneo mengine yote”.

Akafafanua kuwa: “Opresheni ya kufanya usafi inahusisha barabara za pembezoni na katikati ya mji pamoja na viwanja vya wazi vilivyopo pembezoni mwa barabara, tumeweka muda maalum ya kufanya kazi hiyo, tumepanga kufanya kazi siku saba hadi kumi tuwe tumemaliza kusafisha eneo la chuo kikuu cha Karbala na barabara ya (Baabil – Karbala), (Najafu – Karba), (Bagdad – Karbala), jumla ya watumishi 25 wanafanya kazi kila siku wakiwa na magari maalum ya taka”.

Akasema: “Hatua ya kwanza itahusisha kusafisha eneo la (Baabu – Karbalaa) hadi kwenye Maahadi ya ufundi, kazi itaendelea hatua kwa hatua hadi tumalize kusafisha barabara zote zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: