Mhadhara wa kisayansi kuhusu siku ya sukari duniani

Maoni katika picha
Kitivo cha udaktari katika Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeratibu na kutoa mhadhara wa kisayansi kuhusu ugonjwa wa sukari na namna ya kujikinga nao pamoja na njia za kujitibu, kutokana na kuadhimisha siku ya sukari duniani, umetolewa na mkufunzi Dokta Samiri Hassan Rikabi na kuhudhuriwa na kundi la walimu, wanafunzi na wafanyakazi wa chuo kwa lengo la kujenga uwelewa wa kujikinga na maradhi ya sukari.

Amezungumzia mambo mengi katika mada yake, ikiwa ni pamoja na kuangazia uwelewa wa maradhi ya sukari na aina zake, na kuhimiza mlo wa kuzingatia afya pamoja na umuhimu wa kufanya mazowezi kila siku.

Tambua kuwa siku ya kimataifa ya maradhi ya sukari, ni siku ya kueleza hatari za maradhi hayo na huadhimishwa dunia nzima katika siku kama ya leo kila mwaka, kuanzia siku kama leo safari ya kupambana na maradhi hayo huanza na kuendelea mwaka mzima, siku hii ilipangwa na umoja wa mataifa kupitia shirika la afya duniani, ikiwa kama kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Fedrek Pantong aliye gundua Insulin mwaka 1922 ambayo ndio sababu ya kuendelea kuwepo kwa maradhi ya sukari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: