Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya wahadhiri wa Husseiniyya, imefanya majlisi rasmi ya kuomboleza tukio hilo adhim, majlisi hiyo itaendelea kwa muda wa siku sita.

Kiongozi wa idara hiyo Shekh Swahibu Twaaiy ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Idara imezowea kufanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kila mwaka, majlisi itafanyika kwa muda wa siku sita ndani ya ukumbu wa haram ya ukarimu, mhadhara wa kwanza umetolewa jana na itaendelea hadi Ijumaa (27/11/2020m)”.

Akaongeza kuwa: “Ndani ya siku zote sita kutakuwa na majlisi za asubuhi na jioni, wazungumzaji watakua ni Shekh Basim Wahili, Shekh Bilali Qabasi, Shekh Salaam Askariy na Sayyid Hadi Twawirujawi”.

Akaendelea kusema: “Mada zitakazo tolewa katika majlisi hizo zitahusu uhai wa bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake katika uislamu pamoja na kueleza utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w), bila kusahau dhulma aliyo fanyiwa katika maisha yake matukufu”.

Akasema kuwa: “Majlisi hizi zitahitimishwa kwa kuzungumzia kifo cha bibi Fatuma Maasumah (a.s)”.

Akafafanua kuwa: “Tumechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona wakati wa majlisi ikiwa ni pamoja na ukaaji wa umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu”.

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu wa kifo cha mtoto wa Mtume bibi Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake, jambo hilo linaonyesha dhulma aliyo fanyiwa hadi akaamua kumhusia mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche kaburi lake wala jeneza lake lisishuhudiwe na mtu aliye mdhulumu, kuchukia ilikuwa haki yake. Wakati wa kifo chake alikua na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: