Kuweka mazingira ya huzuni za kifo cha Fatuma (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuataia kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza inayo sema alikufa mwezi nane Rabiul-Aakhar.

Atabatu Abbasiyya tukufu na korido zake zimewekwa mapambo meusi na kuta zake zimefunikwa vitambaa vyeusi vilivyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni katika kukumbuka kifo chake.

Kama kawaida; Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza msiba huu, idara ya masayyid itafanya majlisi za kuomboleza kwa muda wa siku tatu, na idara ya wahadhiri wa kike itafanya majlisi kwa muda wa siku sita asubuhi na jioni, pia kutakuwa na majlisi maalum ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), itakayo fanywa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya ukumbi wa utawala.

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu wa kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya nyingi kuhusi tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), hii inaonyesha ukubwa wa dhulma aliyo fanyiwa, hadi akampa usia mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche sehemu ya kaburi lake na jeneza lake lisishuhudiwe na mtu yeyote miongoni mwa wale walio dhulumu haki yake, alikufa akiwa na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: