Kuanza kwa ujenzi wa eneo la mlango wa Bagdad (Baabu-Baghdad).

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu na wenzao wa ofisi ya mkoa wa Karbala wameanza hatua ya awali ya mradi wa ujenzi wa eneo la mlango wa Bagdad (Baabu-Bagdad) unao elekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kurahisisha matembezi wa mazuwaru hususan kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya ujenzi katika kitengo tajwa, Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil amesema: “Kazi imehusisha kutoa vizuwizi vyote vilivyo wekwa na askari na kuhamishia sehemu nyingine, kazi hiyo ipo katika hatua ya mwisho baada ya kufanya vikao mbalimbali vya kujadili ujenzi huo, tunatarajia kuwa eneo hilo litakua lango la mfano lenye uzuri unao endana na sehemu hiyo, ukizingatia kuwa hiyo ndio sehemu pakee ya kuingilia mazuwaru wanaotoka Bagdad”.

Akaongeza kuwa: “Ramani imeandaliwa na jopo la wataalamu wa chuo kikuu cha Karbala, inaupanuzi wa barabara na kuondoa vizuwizi vya ukaguzi, na kutosheka na sehemu za kukagulia watu peke yake na kuongeza mapambo”.

Kumbuka kuwa mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na mafundi wa idara ya mkoa wa Karbala pamoja na wadau wengine hapa mkoani, wanafanya kazi kwa kushirikiana muda mrefu katika miradi inayo saidia kuhudumia mazuwaru, walianza na mradi wa kukarabati na kutengeneza barabara za mji mkongwe pamoja na barabara zingine kwa ajili ya kurahisisha matembezi ya mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: