Maahadi ya Quráni/ tawi la Bagdad inaendelea na harakati zake na inatoa semina mbalimbali

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya imeanza kutoa semina za Quráni kwa kuhudhuria wanafunzi darasani.

Semina hizo zimeanza kufanywa baada ya vikao kadhaa vilivyo jadili haja ya wanafunzi kuingia darasani baada ya kusimama jambo hilo kutokana na janga la korona, na kubakia ufundishaji wa kutumia mitandao (elimu masafa), uwepo wa mwanafunzi darasani huongeza uwezo wa kuelewa soma.

Tawi limetangaza kufungua semina za kuhifadhi Quráni, hukumu za Quráni na tajwidi, jumla ya semina (10) zitafanywa katika mji wa Raswafa, na (12) katika mji wa Karkha chini ya walimu waliobobea kwenye masomo ya Quráni, vifaa vyote vya kujikinga na maambukizi ya Korona vimeandaliwa, sambamba na kupanga ukaaji wa umbali unaotakiwa kiafya kati ya mtu na mtu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya huwapa wanafunzi wake semina mbalimbali za Quráni tukufu kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: