Mbele ya malalo ya mtoto wake na ndugu yake: Mawakibu za kuomboleza zinaadhimisha kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu tangu asubuhi ya leo mwezi (8 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (24 Novemba 2020m), zimekuwa zikipokea mawakibu za waombolezaji zinazo kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na msiba mkubwa uliotokea kwenye nyumba ya Mtume na mashukio ya wahyi katika siku kama ya leo mwezi nane Rabiul-Aakhar mwaka wa 11 hijiriyya, kwa kufa kishahidi bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza.

Kuomboleza msiba huu ni jambo lililo zoweleka kufanywa na watu wa Karbala, sawa iwe ni katika kumbukumbu ya kifo hiki, au kifo cha mmoja wa Maimamu watakasifu (a.s), wamerithishana kizazi baada ya kizazi.

Tambua kuwa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeweka utaratibu wa kupokea mawakibu zinazokuja kuomboleza msiba huu, kimepanga njia watakazo pita na kituoa cha kuanzia matembezi, pamoja na kuzingatia masharti yote ya afya na kuyafanyia kazi, na kuhakikisha hautokei msongamano wala muingiliano baina yao, kuanzia mwanzo wa matembezi hadi mwisho.

Kumbuka kuwa mawakibu zinatumia barabara zinazo elekea kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamesimama kwa mistari na kuimba kaswida za kuomboleza msiba huu, huku wanatembea hadi kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga vifua vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: