Idara ya Quráni inafanya shindano la (Khalaful-ula min khairul-wara) shindamo maalum la wanawake

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake linalofungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya limeanza shindano la (Khalaful-ula min khairul-wara) linalo fanywa kwa njia ya mtandao kwa wanawake, shindano hili ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Askariy (a.s).

Kiongozi wa idara Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Shindano hili linahusu historia ya Imamu Askariy (a.s) iliyo andikwa katika kitabu cha A’laamul-Hidaya kwenye juzu maalum kuhusu Imamu Hassan Askariy (a.s), na yaliyo andikwa ndani ya kitabu hicho kuhusu matukio ya kipindi cha uhai wake (a.s), mambo yatakayo ongeza uwelewa wa historia kwa washiriki na kuwajulisha mambo muhimu kitamaduni na kihistoria”.

Akaongeza kuwa: “Wamepewa muda wa kutosha wa kusoma kitabu hicho kwa ajili ya kushiriki shindano, na tutatoa zawadi kwa washindi baada ya kuyapigia kura majina ya watakaojibu vizuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: