Kwa upasuaji wa ainayake: Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kuondoa uvimbe kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka sitini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kuondoa uvimbe uliokuwa umeota kwenye mgongo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka sitini.

Taktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya rufaa Alkafeel ambaye ni raia wa Sirya, Dokta Waaili Qassim amesema kuwa: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kuondoa uvimbe uliokuwa umeota kwenye mgongo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka (62), chini ya uangalizi wa kifaa-tiba cha kisasa”.

Akabainisha kuwa: “Uvimbe huo ulisababisha udhaifu mkubwa kwa mgonjwa kiasi alikuwa hawezi kuzumia haja yake”.

Akaongeza kuwa: “Mgonjwa alikuwa amesha kwenda kwenye hospitali nyingi na kukutana na madaktari wengi, na alifanyiwa upasuaji bila mafanikio”.

Akafafanua kuwa: “Madaktari walikuwa wanaona sababu ya ugonjwa wake ipo kwenye uti wa ngongo (lumbar vertebrae)”.

Akasema kuwa: “Baada ya kumfanyia vipimo tulibaini tatizo lake, na tumemfanyia upasuaji wenye mafanikio na sasa hivi anaendelea na matibabu ya kawaida, na afya yake inatarajiwa kuimarika na kurudi katika hali ya kawaida”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa wa ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya kutoa ushindani mkubwa kwenye hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila baada ya muda fulani, sambamba na kupokea wagonjwa mbalimbali walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: