Vyanzo vya fikra na sifa za manhaji ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu: Anuani ya mhadhara wa kifikra unaofanywa na chuo kikuu Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya nadwa chini ya anuani isemayo (vyanzo vya fikra na sifa za manhaji ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani –d.i-) iliyo hudhuriwa na kundi la wasomi wa kisekula na viongozi wa jamii na Dini.

Mzungumzaji wa nadwa hiyo alikuwa ni Dokta Hussaam Ali Hassan Abidi, amezungumza misingi muhimu anayo tumia Marjaa Dini mkuu katika kuamiliana na mambo ya kisiasa, pamoja kutoingilia kwa undani kazi za kisiasa, na kuelekeza watu waishi kwa amani katika jamii, na umuhimu wa kuandikwa katiba na mikono ya wairaq waliochaguliwa kuwakilisha tabaka zote za jamii za wananchi wa Iraq.

Katika nadwa hiyo Abidi amebainisha kuwa: “Nadwa hii ni sehemu ya harakati za chuo kikuu cha Alkafeel za kutoa huduma kwa vikundi tofauti vya jamii, kufuatia maombi ya makundi hayo miongoni mwa wakazi wa Bagdad”.

Washiriki wa nadwa wametoa shukrani kwa chuo kikuu cha Alkafeel kutokana na harakati zake za kuwajenga vijana na kuwafundisha tabia njema na uzalendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: