Idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendesha opresheni ya kupima virusi vya Korona kwa watumishi wa Ataba, kwa ajili ya kulinda afya ya watumishi na mazuwaru, kila siku watapimwa watumishi (50) hadi (100) chini ya ratiba maalum iliyo pangwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala.
Kutokana na maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Dokta Osama Abdul-Hassan, amesema kuwa: Atabatu Abbasiyya tangu siku za kwanza za maambukizi ya virusi vya Korona, imekuwa mstari wa mbele kuchukua tahadari za kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo, na kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake na mazuwaru, imeunda kamati maalum ya kusimamia utekelezaji wa hatua za kujikinga na maambukizi, miongoni mwa majukumu ya kamati hiyo ni kufanya opresheni za aina hii zinazo saidia kugundua watu walio ambukizwa ambao bado athari za maradhi hazijaanza kudhihiri kwao na kupunguza uwezekano wa kuugua.
Akabainisha kuwa: Opresheni inafanywa ndani ya ukumbi wa kituo cha Ummul-Banina (a.s), chini ya madaktari waliobobea, watumishi wanaopewa huduma ni kati ya (50) hadi (100) kwa siku, huchukuliwa sampo zao na kupelekwa katika kituo cha (Pcr) kisha huletewa majibu ya vipimo vyao, halafu huchukuliwa hatua inayo fuata kutokana na majibu yaliyo patikana.
Akamaliza kwa kusema: Sambamba na kuwapima, tunatoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na maradhi mengine ya kuambukiza, na kuwahimiza washikamane na maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya.