Atabatu Abbasiyya tukufu imekaribisha vijana 80 wa Basra

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha utamaduni Alqamaru chini ya kitengo cha elimu na utamaduni imepokea vijana 80 wa Basra katika ratiba ya msimu wa (Multaqal-Qamaru thaqafi), kwa ajili ya kuongeza maarifa kwa vijana, kwa kuangalia mambo yaliyopa katika jamii kwa sasa.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kitengo Shekh Harithi Dahi amesema: “Tumepokea hawa vijana baada ya kuwasiliana na Mu’tamad Marjaiyya pamoja na muwakilishi wa Multaqa katika miji yao, ambao ni sehemu ya ratiba ya kukaribisha makundi ya vijana kutoka mikoa tofauti chini ya utaratibu maalum na kusimamiwa na jopo la wataalam wanao endana na aina na umri wa vijana wanao alikwa”.

Akaongeza kuwa: “Ugeni wa vijana hao ulikua makundi mawili, kundi la kwanza kutoka wilaya ya Harithah katika mkoa wa Basra, na kundi la pili kutoka maeneo tofauti ya mkoa huo, baada ya kukaribisha mradi huu na malengo yake na kushiriki kwenye semina zilizo fanywa na Multaqa, tumeandaa ratiba yenye vipengele vingi vinavyo endana na kikundi kusudiwa, kwa kuzingatia kiwango cha waalikwa”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba ambayo wamehudhuria vijana hawa ina mihadhara ya kifikra, kiitikani, maendeleo ya binaadamu pamoja na kutembelea baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mengineyo”.

Kumbuka kuwa Multaqal-Qamaru ni mradi unaolenga vijana wa aina tofauti katika jamii, kwa lengo la kuwasaidia kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii kwa kutumia elimu za kisasa bila kujenga chuki na mifarakano katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: