Kituo cha uokozi na huduma ya kwanza Alkafeel kinatoa mafunzo kwa watumishi wa moja ya hospitali za Karbala

Maoni katika picha
Kituo cha uokozi na huduma ya kwanza Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya kimeandaa semina kwa watumishi wa hospitali ya Abu Mahadi Muhandisi katika mkoa wa Karbala, kupitia harakati zake zinazo lenga kutoa huduma ya uokozi na matibabu, kwa ajili ya kupunguza hasara na maumivu, sambamba na uokozi wa haraka pindi linapo tokea janga lolote.

Kwa mujibu wa mkuu wa kituo hicho Ustadh Murtadha Ghalibi amesema kuwa: “Semina hii ni sehemu ya mfululizo wa harakati za utowaji wa mafunzo, ambayo tumekuwa tukitoa kwa makundi mbalimbali likiwemo kundi hili la madaktari, semina hii inayo fanywa chini ya anuani isemayo (kulinda roho katika msikiti mtukufu), inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - (Katika kila nyumba inayo okolewa) inalenga namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu mwenye tatizo la moyo kwa mkubwa na mtoto ambae bado ananyonya na namna ya kumlinda mhusika.
  • - Utaratibu wa (huduma ya kwanza) nao ni njia za uokozi na huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa kisukari, pamoja na njia za kumhudumia mgonjwa wa kisukari.

Akabainisha kuwa: “Masomo ya semina hii yanatolewa kwa njia ya nadhariya na vitendo, ili kurahisisha uwelewa kwa washiriki na kuwawezesha kutoa huduma yeyote inayo hitajika wakati wa uokozi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu muitikio ni mzuri kutoka kwa washiriki”.

Kumbuka kuwa kituo cha uokozi na huduma ya kwanza Alkafeel kinategemewa na maahadi ya afya (ASHI) katika kutoa mafunzo ya uokozi kwa makundi tofauti katika jamii, kimesha fundisha mamia ya watu ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya uokozi kutokana na mafunzo waliyo pewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: