Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na rais wa kitengo cha uhusiano Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema kuwa, Atabatu Abbasiyya imesimama imara kupambana na kila janga au kimbunga kinachotaka kuharibu harakati za maisha ya wananchi, likiwemo janga la Korona linalo tishia maisha ya raia wa Iraq na mataifa mengine.
Yamesemwa hayo katika ujumbe ulio wasilishwa kwa niaba ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwenye hafla ya kutoa zawadi iliyo andaliwa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu chini ya kitengo cha mahusiano, ambapo yametangazwa majina ya washindi wa shindano la (ubao wa uhai) lililo husisha wanafunzi wa sekondari (upili), lililofanywa asubuhi ya leo mwezi (12 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (28 Novemba 2020m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).
Akasema: “Ataba tukufu inanafasi kubwa katika kupambana na kirusi hiki hatari, inapambana kila upande, ukianzia upande wa kinga; imekuwa ikipuliza dawa kwenye masoko, nyumba za makazi ya watu, nyumba za kutoa huduma za kijamii kama vile mahospitali, yote hayo ni kwa ajili ya kuzuwia maambukizi na daima wamekua mstari wa mbele katika vita hii”.
Akasisitiza kuwa: “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya ni jeshi imara dhidi ya virusi vya Korona na limesaidia kulinda maisha ya watu wengi, shindano hili ni uwanja mwingine wa kuonyesha kazi nzuri zilizo fanywa katika kupambana na majanga na kuleta matumaini kwa raia wa Iraq, sambamba na kuonyesha ukarimu wa wairaq, watumishi wetu wamejitolea mali zao na maisha yao kwa ajili ya wananchi wa taifa lao, wakiwemo madaktari ambao wanaitwa jeshi leupe, wameonyesha kwa vitendo jinsi ya kufanya kazi kwa uaminifu na kujtolea wakati wote, Mwenyezi Mungu awahifadhi waliobaki hai miongoni mwao na awarehemu walio fariki”.
Akamaliza kwa kusema: “Tunawashukuru wasimamizi wa shindano hili pamoja na wasimamizi wa shule kutoka wizara ya malezi na taasisi ya Najafu-Alkhairiyya, pamoja na harakati ya wanamichezo wa Bagdad, tunashukuru watu wote walio shiriki kwenye shindano hili, kwani wamehuisha moyo wa kujitolea kwa mara nyingine na shukrani za pekee ziende kwa kila aliye saidia kufanikiwa kwa shindano hili, Mwenyezi Mungu atawalipa hakika yeye ni mbora wa walipao”.