(Soma na tambua) App inayotimiza malengo yako ya usomaji wa Quráni tukufu kwa ufasaha na tafsiri yake

Maoni katika picha
App ya (soma na tambua) iliyo tengenezwa na idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini kitengo cha wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni App iliyo pangiliwa vizuri na raisi kuitumia, inamuwezesha mtumiaji kusoma Quráni kwa ufasaha pamoja na tafsiri yake, yakiwemo masomo ya Fiqhi na malezi yatokanayo na kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.

App hii ni kwa ajili ya kuimarisha usomaji wa Quráni tukufu na kuitafakari, mtu mwenye kuitumia itamtoshelezea kupeba kitabu cha Qurán, aidha ni rahisi kuwa nayo popote ulipo, inasauti na picha za aya za kitabu cha Mwenyezi Mungu kitakatifu.

Miongoni mwa huduma zinazo patikana katika App hiyo ni:

  • Unaweza kusoma Quráni pamoja na watu wengine kutoka kila sehemu ya dunia.
  • Inamasomo ya Fiqhi, Quráni, malezi na inamuongoza msomaji kusoma kwa usahihi.
  • Inamjulisha mtumiaji wake malipo anayopata duniani na akhera, pamoja na uombezi siku ya kiyama.
  • Kuna washiriki mia moja na hamsini (150) wa usomaji wa Quráni kila siku, ndani ya miezi mitano.
  • Inamuwezesha mshiriki kufanyiwa ziara kwaniyaba.
  • Inampa nafasi mshiriki kushiriki mara ya pili katika usomaji wa Quráni kama akitaka, na kwa muda unaomfaa.

Kwa mujibu wa tuliyosema; ushiriki wa kusoma Quráni kila siku, mtumiaji anatakiwa kusoma japo (robo ya hizbu) kwa muda wa miezi (5) ataweza kumaliza Quráni tukufu, kama akifanikiwa kujisajili katika washiriki 150 kwenye kila usomaji.

Unaweza kujisajili kupitia njia zifuatazo:

Kwanza: Simu zote za kisasa -smartphone- (IOS).

Pili: Simu zote za kisasa -smartphone- (Android).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: