Idara ya utafiti katika kituo cha turathi za Hilla inaendelea na kazi ya kuhuisha turathi za Hilla

Maoni katika picha
Idara ya utafiti katika kituo cha Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa idara muhimu katika kituo hicho, kutokana na ukubwa wa kazi zake, kuanzia uandishi, uhakiki na uchambuzi wa tafiti na vitabu vinavyo tolewa na kituo hicho, hufanya marekebisho katika ngazi zote, ngazi ya lugha, nahau na mpangilio wa maneno, sambamba na aina ya uchapishaji na kuhakikisha kitabu kinakuwa na muonekano mzuri, mkuu wa kituo cha turathi za Hilla Shekh Swadiq Khuyalidi amesema kuwa: “Idara ya tafiti ni sawa na uti wa mgongo katika ofisi ya uhakiki, ndio msingi wa kuwepo kwa kituo na utambulisho wake, miongoni mwa kazi zinazo fanywa na kituo ni: kutoa jarida la (turathi za Hilla) lililojaa tafiti za kielimu, kutoa jarida la (Radu-Shamsi) lililojaa Makala kuhusu wanachuoni wa Hilla, kuhakiki na kukagua vitabu vyote vinavyo andikwa na kituo”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa vitabu vilivyo andikwa na kituo hiki ni: Mausua Asri Ilmiyyatu Hilla, Mu’jamu Mu-Arikhi Hilla, Mu’jamu Nasakhi Hilliyyina, Hillatu fi kutubi Rahalah, Darsu Nahawiyyu fi Hilla pamoja na vitabu vingine vingi ambavyo vitatolewa hivi karibuni, aidha kituo kilisimamia (shindano la kitabu cha Hilla)”.

Kumbuka kuwa idara ya utafiti katika kituo cha turathi za Hilla ni miongoni mwa idara muhimu, inayo fanya kazi ya kuhuisha turathi za Hilla na kuziweka katika mfumo wa elimu na tafiti, na kuwa kimbilio la watafiti wa mambo yanayohusiana na turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: