Kukamilika kwa mchoro wa dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) na kuanza maandalizi ya utengenezaji

Maoni katika picha
Kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya kuweka kwenye makaburi matukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kukamilika kwa mchoro wa dirisha jipya la bibi Zainabu (a.s) baada ya kufanya usanifu mara kadhaa wa dirisha hilo.

Haya yamesemwa na rais wa kitengo tajwa Sayyid Naadhim Ghurabi, amesema: “Baada ya kupewa kazi ya kutengeneza dirisha la bibi Zainabu (a.s), watumishi wetu walianza kufanya upembuzi yakinifu na kutengeneza mchoro wa dirisha hilo, walitengeneza zaidi ya mchoro mmoja, baada ya majadiliano kati ya Atabatu Abbasiyya na Ataba ya bibi Zainabu (a.s) yakafikiwa makubaliano ya kupasisha moja ya michoro hiyo, kwa ajili ya kuendelea hatua ya utengenezaji, dirisha hilo litakuwa na uzuri wa hali ya juu, mambo mengi yamezingatiwa katika dirisha hilo hususan sehemu ya juu ambayo ilitengenezwa na mafundi wetu siku za nyuma pamoja na kuwa na uwiyano na dirisha la zamani na la sasa pamoja na kuwa na baadhi ya sifa zilizopo kwenye dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Hatua ya kuandaa mchoro huzingatiwa kuwa hatua muhimu ya kuelekea katika utengenezaji, siku zijazo tutaanza kutumia mchoro huo na kutengeneza dirisha halisi, chini ya ratiba maalum ya mradi, tayali vifaa vyote vimesha fika, mbao na madini (dhahabu, fedha na silva) kazi itafanyika kama ilivyo pangwa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kazi itakamilika hatua baada ya hatua, mafundi watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanakamilisha mradi kwa wakati uliopangwa, na itaingizwa katika orodha ya kazi zilizo fanywa kwa mafanikio katika kiwanda hiki, tena kwa kufanywa na raia wa Iraq na watumishi wa Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kuwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaofanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza madirisha ya makaburi na mazaru matukufu, wanauzowefu mkubwa wa kufanya kazi hiyo, wameweza kuonyesha mafanikio yao pale walipo tengeneza dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na madirisha ya Maqaamu Swafi-Swafa bila kusahau dirisha la Qassim (a.s) na milango ya malalo ya Sayyid Muhammad –Sabú-Dajaili- na dirisha la malalo ya Shekhe Mufidi na Shekh Tusi, na sehemu ya juu ya dirisha la Maimamu mawili Jawadaini (a.s) pamoja na kazi zingine nyingi, ikiwemo kazi ya kutengeneza dirisha la mbele ya Maqamu ya Imamu Mahadi (a.f) pamoja na paa na taji la dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) pamoja na kazi inayo endelea hivi sasa ya kutengeneza dirisha la Maqaamu ya mkono na upande wa dirisha la Maqaamu sehemu ya wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: