Hashdu-Atabaat imekusudia kufanya kongamano la kwanza

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Hashdu-Atabaat ni walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa), viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s) na Ali Akbaru (a.s) na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answaaru-Marjaiyya wamekusudia kufanya kongamano la kwanza siku ya Jumanne (15 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (1 Desemba 2020m) litakalo dumu kwa muda wa siku tatu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kituo cha habari, kongamano hilo litafanyika siku moja katika Atabatu Alawiyya tukufu na siku mbili katika Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, wakati wa kongamano hilo ulinzi na usalama utaimarishwa, pamoja na mfumo wa mawasiliano, tunatarajia kualika viongozi mbalimbali, kongamano litahitimishwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Alkhamisi mwezi (17 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (3 Desemba 2020m), kikao cha kufunga kongamano kitakuwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwasilishwa maazimio ya kongamano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: