Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya shindano kwa wanawake ambalo wamelipa jina la (nyumba ya Fatuma) litakalo fanyika kwa njia ya mtandao, kama sehemu ya kukumbuka kifo cha bibi Zaharaa (a.s) na kuomboleza msiba huo mkubwa.
Kiongozi wa kituo bibi Asmahani Ibrahimu amesema kuwa: “Hakika shindano hili ni sehemu ya mashindano ambayo hufanywa na kituo chetu katika kuadhimisha tarehe za kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu (a.s), likiwepo tukio hili, tunategemea shindano hili kuwa mlango wa kuonyesha uwezo wa wanawake, na uwe mwanzo wa kusonga mbele”.
Akaongeza kuwa: Ushiriki utakuwa huru na hautajibana kwenye mada maalum, ukizingatia kuwa huyu ni mtu mtukufu, tunaweza kuchota mambo mengi kutoka kwake, lakini mshiriki anatakiwa aandike mada moja tu atakayo chagua.
Asmahani akaendelea kusema: “Tutaendelea kupokea mada za washiriki hadi siku ya Jumanne (22 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (8 Desemba 2020m), mada zitumwe kwenye mtandao ufuatao: https://t.me/Thaqafaasria pamoja na majina matatu ya mshiriki/ jina la mkoa na/ namba ya simu, zawadi za washindi watakao tangazwa majina yao zimeandaliwa”.