Idara ya Quráni tawi la wanawake chini ya ofisi ya maelekezo ya dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Khalaful-ula min khairul-wara) lililofanywa katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Askariy (a.s) na kupata ushiriki wa watu (125).
Kiongozi wa idara bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano limepata muitikio mkubwa, washiriki wametoka mikoa tofauti, kila mshiriki alitakiwa kusoma kitabu chenye kurasa (200) kwa ajili ya kuingia kwenye shindano”.
Akabainisha kuwa: “Lengo kuu la shindano hili ni kuangazia historia ya Maasumina (a.s) na yaliyotokea katika uhai wake na kuongeza maarifa ya kuwatambua Ahlulbait (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Aidha idara ya Quráni inatoa shukrani ya dhati kwa wakina dada wote walioshiriki na tunawaombea mafanikio mema, pongezi za pekee ziwafikie wakina dada wote baada ya kupata ushindi mkubwa”.