Kengele ya kuingia darasani imepigwa tena katika shule za Al-Ameed

Maoni katika picha
Kengele ya kuingia darasani imepigwa upya katika shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kama tangazo la kuanza mwaka mpya na safari ya kuingia hatua nyingine ya masomo, chini ya mazingira tulivu yanayo zingatia masharti yote ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kutokana na tukio hili Dokta Ahmadi Kaabi rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu amesema kuwa: “Shule za awali za Al-Ameed zimeanza kupokea watoto katika mazingira yaliyojaa shangwe na furaha, kwa kuondoka kwao katika malezi ya familia na kuja kwenye malezi ya shule, na kuanza ukurasa mpya katika maisha yao, masharti yote ya afya yamezingatiwa, ikiwa ni pamoja na ukaaji wa umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu na kuweka barakoa na mengineyo”.

Kaabi amewahakikishia wazazi usalama wa watoto wao, shule za Al-Ameed zinatoa malezi na elimu katika mazingira bora kiafya na kijamii, zinawaandaa kikamilifu kwa ajili ya kuingia katika shule za msingi.

Ustadh Wasim Abdulwahidi kiongozi wa idara ya elimu amewema kuwa: “Kitengo cha malezi na elimu ya juu kimeanza kutekeleza ratiba ya (wiki ya kuishi kwa amani), inayolenga kuwazowesha wanafunzi mazingira mapya, ili wazoweane pamoja na watoto wengine”.

Akafafanua kuwa: “Wiki ya kwanza katika mwaka wa masomo ya shule za awali huwa tunakuwa na ratiba ya (wiki ya kuishi kwa amani), kwa ajili ya kuwabadilisha kudogo kidogo kutoka mazingira ya nyumbani na kuingia mazingira ya shule, na kuwalea kinafsi na kijamii kwa kuweka mazingira ya urafiki baina yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: