Kituo cha uandaaji wa vipindi na matangazo mubaashara Alkafeel kimeandaa masafa ya kurusha kongamano la Hashdu-Atabaat la kwanza

Maoni katika picha
Kituo cha habari cha kongamano la Hashdu-Atabaat chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuandaa masafa ya kurusha matukio ya kongamano katika siku ya kwanza, litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Hashdu-Atabaat walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa), linalo simamiwa na viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answaru Marjaiyya, siku ya Jumanne mwezi (15 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (1 Desemba 2020m) saa nne asubuhi na litaendelea kwa muda wa siku tatu.

Wametoa wito kwa vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyo penda kurusha matukio ya kongamano hilo, watumie anuani zifuatazo:

Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A)

DOWNLINK:12680.200 H

MOD:DVBS2

QPSK

FEC:5/6

Sr :3250

HD/MPEG-4


Ratiba ya matangazo itakuwa kama ifuatavyo:

  • 1- Usomaji wa Quráni tukufu.
  • 2- Wimbo wa taifa la Iraq na kusoma surat Fat-ha.
  • 3- Kukaribisha wageni (Uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu).
  • 4- Ujumbe kutoka kwa Ustadh wa Hauza, Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum.
  • 5- Video inayo onyesha ushujaa na kuanzishwa kwa vikosi vinne.
  • 6- Ujumbe kutoka wizara ya ulinzi.
  • 7- Ujumbe kutoka kwa vikosi vya Hashdu-Atabaat.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: