Toleo la kumi na moja katika jarida la kielimu Albaahiru

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa jarida la kumi na moja kwa idadi mbili (ishirini na moja na ishirini na mbili) la elimu ya mazingira na uhandisi Albaahiru, limejaa tafiti mbalimbali (zipatazo saba) kwa lugha ya kiengereza.

Kamati ya wahariri wa jarida imesema kuwa: Miongoni mwa mambo yanayo tarajiwa na kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat ni kugundua mambo na kuyaendeleza, kama sehemu ya kushajihisha ufanyaji wa tafiti wa kielimu na kihandisi, na kuandika matokeo ya tafiti hizo katika jarida hili, jarida hili ni maalum kwa ajili ya kuandia matokeo ya tafiti mbalimbali, tolea la sasa limeandika matokeo ya utafiti wa kemia ya viumbe hai, fizikia na uhandisi wa majengo.

Akaongeza kuwa: tunatarajia tafiti hizi zimalize kiu ya msomaji na zifungue milango ya watafiti, kwa kuandika tafiti zingine kupitia kilicho andikwa katika jarida hili.

Mwisho jarida limetoa wito kwa watafiti wote wa fani tofauti, wachangie kupitia tafiti zao uboreshaji wa elimu na maarifa, jambo ambalo ndio lengo kubwa la jarida hili, na ndio msingi wa kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: