Kufanyika kwa kikao cha kwanza katika kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya Jumanne mwezi (15 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (1 Desemba 2020m) katika Atabatu Alawiyya tukufu, kimefanyika kikao cha kwanza katika kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza linalo simamiwa na viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answaru Marjaiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (Hashdu Atabaat walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa).

Kuhusu warsha hiyo msemaji wa kongamano Ustadh Hazim Fadhili ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Katika siku ya kwanza tumefanya kikao cha kutambuana, kilicho husisha viongozi wa idara za utawala na mali za kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answaru Marjaiyya”.

Akaongeza kuwa: “Tumejadili mambo tofauti na kubadilishana uzowefu, na kuweka mikakati ya kuwa na mtazamo mmoja wa vikosi hivyo”.

Akaendelea kusema: “Tutakusanya maoni yote yaliyotolewa na tutayachambua kwa kina na kufanya maamuzi ya pamoja”.

Akasema: “Siku mbili zijazo za kongamano pia kutakua na vikao vingine katika Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya tukufu”.

Tambua kuwa kongamano tajwa limeanza asubuhi ya Jumanne katika Atabatu Alawiyya, na kuhudhuriwa na viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama kutoka mkoa wa Najafu Ashrafu na Karbala tukufu, na wawakilishi kutoka ofisi za Maraajii Dini watukufu na viongozi wa Dini pamoja na ujumbe ulio wakilisha Atabatu (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya, Abbasiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: