Kituo cha turathi za Hilla kinaangazia sherehe muhimu katika kitabu cha (Fusulu-Naswiriyya)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatafiti na kuchambua kila kitu kinacho husiana na turathi za Hilla, hususan turathi za kiislamu na wanachuoni wakubwa wa Hilla, wenye mchango muhimu katika uwanja wa elimu, idara ya uhakiki ni njia ya kuhuisha turathi hizo, na sasa inafanya ufafanuzi muhimu wa kitabu cha (Fusulu-Naswiriyya) katika usulu Dini, kitabu hicho kitatoka kwa jina la (Muntaha Su-uul fi sharhi muarabu-fusuul), ni kitabu cha Aqida (ilmu-kalaam), nacho ni msingi hai wa elimu, kimehakikiwa na watumishi wa kituo.

Mkuu wa kituo cha Hilla Shekh Swadiq Khuwiladaya, amesema: “Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu muhimu katika somo la Aqida (ilmu-kalaam) na usulu Dini, nacho ni sherehe muhimu ya kitabu cha (Fusulu-Naswiriyya) katika usulu Dini, vilevile kinaitwa (Alfusuul fil-ilmi usuul), kiliandikwa na Nasru-Dini Tusi (aliyefariki mwaka wa (673h), na asili ya kitabu kilikua katika lugha ya kifarsi, akafanya kazi ya kukikusanya Shekhe Ruknu-Dini Jarjani mwaka (720h), mmoja wa wanafunzi wa Allama Hilliy”.

Akaongeza kuwa: “Sherehe hii inaitwa (Muntaha su-uul fi sharhi muarabu fusuul) cha Shekh Faqihi Maahir Dhwahiru-Dini Ali bun Yusufu bun Abduljaliil Naili Alhilliy wa mwaka (777h), mmoja wa wanafunzi wa Fakharu Muhaqiqi Alhilliy aliyekufa mwaka (771h), Mwenyezi Mungu amuweke mahala patakatifu peponi, watumishi wa kituo chetu wanafanya uhakiki wa vitabu hivyo, karibu watatoa kitabu kamili, kazi imesha kamilika kwa asilimia (%90)”.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Hilla kimesha andika vitabu vingi kuhusu turathi za Hilla, ambavyo ni kimbilio la wanafunzi na watafiti wa turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: