Idara ya mahusiano ya vyuo imepokea ugeni wa walimu wa chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo katika Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea ugeni wa walimu wa chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s) tawi la Baabil, ukiongozwa na mkuu wa chuo Dokta Hassan Jaasim akiwa na jopo la marais wa vitengo vya chuo, wamepokelewa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na msaidizi wa kitengo cha mahusiano.

Tumeongea na kiongozi wa harakati za chuo Sayyid Muntadhiru Swafi kuhusu ziara hiyo, amesema kuwa: “Tumejadili mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufungua ushirikiano kati ya chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s) tawi la Baabil na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kufanya mikutano na makongamano ya kielimu yatakayo ratibiwa na chuo”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mambo mengine muhimu yaliyo jadiliwa ni swala la Atabatu Abbasiyya kuisaidia maktaba kuu ya chuo cha Imamu Alkaadhim, kwa kuipa vitabu mbalimbali, sambamba na kukarabati jengo la chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s) na kujenga paa kwenye baadhi ya maeneo ya chuo”.

Ziara hii ni sehemu ya muendelezo wa ziara za vyuo vya Iraq katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zinazo lenga kuimarisha ushirikiano wa vyuo vya Iraq na Ataba, na kufungua milango ya ushirikiano kwenye sekta ya elimu na utamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: