“Maelekezo ya kidini” ni mada ya nadya ya wazi katika ratiba ya siku ya pili ya kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya siku ya Jumatano mwezi (16 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (2 Desemba 2020m) ndani ya ukumbi wa Sayyid Auswiyaa (a.s) ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu, katika ratiba ya siku ya pili ya kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza, imefanywa nadwa ya wazi na kitengo cha maelekezo ya kidini cha kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi Answaru Marjaiyya.

Nadwa imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Rasulu Al-Aamiriy, ikafuata surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa.

Baada ya hapo likafuata neno la ukaribisho kutoka Atabatu Husseiniyya tukufu lililo wasilishwa na bwana Fadhili Auz, akasema kuwa: “Tunapongeza kuhudhuria kwenu katika kongamano hili ambalo Atabatu Husseiniyya inalipa umuhimu wa pekee, tunafanya makongamano mengi lakini kongamano la -Hashdu Atabaat la kwanza- linalo husisha Hashdu Marjaiyya lina umuhimu mkubwa katika ujenzi wa taifa la Iraq”.

Ukafuata ujumbe wa Hashdu Atabaat ulio wasilishwa na Bulgedia Ali Hamdani kamanda wa kikosi cha Ali Akbaru (a.s) na kiongozi wa opresheni ya Furaat-Ausat katika Hashdu Shaábi, akasema: “Hakika jukumu la kufanyia kazi fatwa ni jukumu la kitaifa, kisheria na kimaadili”.

Akaongeza kuwa: “Hakika kufanyia kazi maelekezo ya Marjaiyya mkuu ni kwa ajili ya amani ya taifa letu, na kulinda ushindi uliopatikana, na mapenzi baina ya wairaq walioleta ushindi na kulinda taifa”.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa maelekezo ya kiitikadi kutoka kikosi cha Ali Akbaru (a.s) uliowasilishwa na Shekh Sahiil Sahiil, miongoni mwa aliyosema: “Katika kipindi muhimu kihistoria na wajibu wa kitaifa, wakati taifa lilipo vamiwa na magaidi, walio mwaga damu na kuharibu maeneo matakatifu, ilitolewa fatwa ya jihadi kifaya kutoka ndani ya haram ya bwana wa mashahidi (a.s), wananchi watukufu wa taifa hili wakajitokeza kwa wingi kuitia wito wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani…”.

Baada ya hapo ikaanza nadwa ya wazi kuhusu nafasi ya maelekezo ya kidini katika Hashdi Shaábi, na njia za kutoa maelekezo hayo katika vikosi vya Hashdu Atabaat.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: