Kongamano la kitamaduni Aljuud linaendelea na ratiba yake mwanzoni mwa mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa chuo na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na ratiba yake kwa kualika wanafunzi wa sekondari na shule za msingi baada ya kuwasiliana na idara ya malezi katika mkoa wa Karbala, wamealikwa wanafunzi kutoka mkoa wa Dhiqaar.

Kiongozi wa harakati za shule Ustadh Mahmudu Qarah Ghauli amesema kuwa: “Kutokana na hali ya kiafya ya sasa tumealika wanafunzi (50) tu, wakati tulikuwa tunaalika wanafunzi wengi zaidi, tumeandaa ratiba ya siku tatu, yenye vipengele vya kitamaduni, kielimu na kimaelekezo, kutakua na mihadhara itakayo tolewa na wasomi waliobobea katika fani hizo, inayo endana na umri wa wanafunzi walio alikwa”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mihadhara muhimu ni ule unaohusu umuhimu wa utamaduni na kuongeza maarifa ya kuutunza, pamoja na kuangazia upotoshwaji unaofanywa na vyombo vya habari, hali kadhalika kuna mihadhara ya dini kuhusu namna ya kuwalinda wanafunzi na changamoto za kijamii, kwa kutumia mwanga wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume (s.a.w.w) pamoja na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa kuangalia mazingira ya maisha ya nyumbani, shuleni na ndani ya jamii, aidha kunamihadhara kuhusu utowaji wa huduma ya kwanza kiafya”.

Akabainisha kuwa: “Tunafanya ratiba za aina hii kwa wanafunzi, ili kuwafanya watambue utamaduni, na kuongeza maarifa katika mambo mbalimbali, pamoja na kuwafundisha namna ya kupambana na mazingira yanayo wazunguka, na kuwapa mbinu za kulinda afya na kutoa huduma ya kwanza ya kiuokozi, na kuhakikisha mwanafunzi anakua mtu bora katika jamii anayo ishi”.

Kumbuka hii ni moja ya ratiba za idara ya mahusiano ya vyuo vikuu, chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, baadhi ya watumishi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya wanashiriki kwenye ratiba hii kulingana na fani zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: