Toleo la jarida la saba katika majarida ya turathi za Karbala

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa toleo la (tatu na la nne) la jarida la saba katika majarida ya turathi za Karbala ya kielektronik.

Vitabu hivyo vimejaa tafiti za aina mbalimbali, kuna jumla ya tafiti kumi na nne, ukiwemo utafiti kuhusu mwanachuoni mashuhuri wa karne ya tisa na kumi hijiriyya, Shekh Taqi-Dini Ibrahim Kafámi Al-Aamiliy aliye fariki mwaka (905h) katika mji wa Karbala, baada ya kuishi hapo miaka kumi na tano, mwanachuoni huyo alikua bingwa wa Fiqhi na Hadithi pia alikua mwenye zuhudi na taqwa, alijulikana kwa kuandika vitabu vingi, anavitabu vya masomo tofauti, tumeandika tafiti tatu na ujumbe ulio hakikiwa.

Unaweza kuangalia majarida yote na kupakua kutoka kwenye toghuti ya wizara ya elimu ya juu kupitia link ifuatayo: https://www.iasj.net/iasj/issue/11740

Au kwenye toghuti ya turath@alkafeel.net

Kwa kushiriki: tuma tafiti kwenye anuani hii drehsanalguraifi@gmail.com. Au kwenye toghuti ifuatayo: http://karbalaheritage.alkafeel.net/ au peleka moja kwa moja katika ofisi za jarida zilizopo: (Iraq/ Karbala/ mtaa wa Baladiyya/ mkabala na hoteli ya Baitul-Juud/ karibu na taasisi ya Maásumina kumi na nne –a.s-).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: