Mawakibu Husseiniyya zimeanza kupuliza dawa mashuleni

Maoni katika picha
Kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuwa; mawakibu zimeanza kupuliza dawa mashuleni, kutokana na kuanza mwaka mpya wa masomo na kusaidia kuweka mazingira salama kiafya kwa wanafunzi, hii ni sehemu ya huduma nyingi zinazo fanywa na mawakibu hizo tangu kuanza kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Idara za mawakibu Husseiniyya katika wilaya ya Madaainu mashariki ya mji mkuu wa Bagdad, wamefanya opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika shule zilizopo eneo hilo, chini ya utaratibu maalum uliopangwa na kwa kutumia dawa stahiki kwa kazi hiyo.

Makamo kiongozi wa idara hiyo Hussein Hassan Mahusi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya kupuliza dawa ni moja ya shughuli zinazo fanywa na mawakibu Husseiniyya, kama sehemu ya kusaidia walimu na kulinda usalama wa afya zao na wanafunzi, kazi hiyo inafanywa kwa kushirikiana na idara za shule wakadi ambao wanafunzi hawapo shuleni, ili kusitokee mgongano kati yetu na wanafunzi, tumepuliza dawa madarasani, sehemu za kupita, na kwenye vyumba vya ofisi pamoja na uwanja wa shule na sehemu za bustani bila kusahau vyooni”.

Rais wa kitengo hicho, bwana Riyadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Mawakibu Husseiniyya zinatoa huduma mbalimbali, kama vile kuhudumia mazuwaru, kutoa misaada na huduma tofauti kwa askari hasa wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh, wanaendelea kutoa huduma mbalimbali katika kupambana na janga la virusi vya Korona, mawakibu zimekuwa zikisimama pamoja na raia daima, kwa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, kama sehemu ya kuitikia wito wa fatwa ya kusaidiana, hali kadhalika wanasaidia watumishi wa afya sambamba na kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi pamoja na kutoa huduma zingine nyingi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: