Kukamilisha semina ya hamsini na moja ya uokozi wa majeruhi vitani

Maoni katika picha
Wataalam wa kituo cha mafunzo ya uokozi na tiba wamekamilisha utoaji wa mafunzo hayo katika semina ya hamsini na moja, semina hiyo imepewa jina la (Ummu Abiha a.s), ambayo wameshiriki wanajeshi, hii ni sehemu ya mafunzo yanayo tolewa na kusimamiwa na wataalam wa uokozi vitani, kwa ajili ya kujenga uwezo wa uokozi kwa wapiganaji, mafunzo haya yanawawezesha kumuokoa majeruhi au mgonjwa katika mazingira yote, jambo ambalo husaidia kupunguza idadi ya vifo (kwa idhini ya Mwenyezi Mungu).

Kiongozi wa mafunzo hayo Sayyid Mustwafa Ghalibi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mafunzo yalikua ya aina mbili (nadhariyya na vitendo), imetolewa mihadhara ya kuelekeza njia za uokozi na kulinda pumzi na utokaji wa damu nyingi pamoja na kulinda joto la muili na majeraha ya kichwani, mihadha imetolewa na watu wenye uzowefu mkubwa wa mambo hayo, sambamba na kuwapa mafunzo ya vitendo”.

Kumbuka kuwa kituo cha mafunzo ya huduma ya kwanza na uokozi, kimesha fundisha makumi ya wanajeshi walio hitimu mbinu mbalimbali za uokozi vitani na kulinda roho zao tukufu, pamoja na kuwatunuku vyeti vinavyo tambuliwa na vituo vya uokoaji vya ulaya, tambua kuwa kituo cha mafunzo ya huduma ya kwanza na uokozi vitani kinakubalika kimataifa ikiwa ni pamoja na vituo vya Ulaya (ESA).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: