Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinahakiki na kuandika faharasi ya kila kinacho husiana na turathi za Karbala kwa kufuata utaratibu bora, hivi sasa kimeanza kuhakiki vitabu vya Mirza Jafari Shaharistani –r.a-. kutokana na umuhimu wa vitabu hivyo ambavyo vinahuisha turathi za kiislamu.
Mkuu wa kituo cha turathi za Karbala Shekh Muhammad Dhwalimi amesema kuwa: “Kituo kinaandika toleo jipya linalo kusanya vitabu vinne vya Mirza Jafari Shaharistani –r.a- ambavyo ni (Usafi wa mtoto wa zinaa, Unajisi wa Ahlulkitabu, Hukumu ya maji ya shaka, Hukumu ya juisi ya zabibu baada ya kuchemka), haya ni mambo muhimu sana katika somo la Fiqhi”.
Akaongeza kuwa: “Watumishi wa idara ya uhakiki katika kituo cha turathi za Karbala wameanza kuhakiki vitabu hivyo, hivi karibuni watatoa toleo maalum, kazi imesha kamilika kwa asilimia zaidi ya (%90)”.
Kumbuka kuwa idara ya uhakiki katika kituo cha turathi za Karbala imesha andika vitabu vingi kuhusu mambo ya turathi, na kuwa kimbilio la wanafunzi na watafiti wa mambo ya turathi.