Hashdu Atabaat tukufu: Watu wote waliitikia fatwa lakini sio wote walio ifanyia kazi… wapiganaji wetu wanamchango mkubwa katika kulinda amani ya taifa

Maoni katika picha
Kamanda wa kikosi cha Ali Akbaru (a.s) Jenerali Ali Hamdani ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: Kila mtu aliitikia fatwa ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani lakini sio kila mtu aliifanyia kazi.

Akaongeza kuwa: Maazimio nane ya kongamano yalikua dira ya utendaji wa vikosi hivi, kuanzia siku ya kunzwa tulishakamana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na bado tunaendelea kushikamana nayo kwa ajili ya kujenga taifa.

Akasema: sisi ni walinzi wa fatwa na watekelezaji wake, kuna watu waliokimbilia madaraka ya vyama, siasa na mengineo.

Akafafanua kuwa: Vikosi hivi vimeshikamana na fatwa hiyo na vimejitolea kupigana jihadi, katika kongamano hili tamko letu limesemwa na mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Maitham Zaidi, kuna ujumbe mwingi uliotolewa na kongamano, Kwanza: kuwapa matumaini raia wa Iraq kutokana na uvunjifu wa amani uliotokea hivi karibuni, kuwa wapiganaji wa Atabaat tupo na tutaendelea kuwa ngome imara katika kulinda taifa na raia kama tulivyo simama imara katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh.

Akaongeza kuwa: kulikuwa na ujumbe pia wa kuendelea kushikamana na fatwa ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani pamoja na maelekezo yake ambayo hutolewa kupitia muwakilishi wake Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: