Semina ya (utendaji bora kiidara) katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na vikao vyake

Maoni katika picha
Semina ya utendaji bora kiidara inayo tolewa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu pamoja na kitengo cha malezi na elimu ya juu wanaendelea na warsha ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakiongozwa na marais wa vitengo pamoja na wakuu wa mashirika.

Semina hii inalenga kuongeza uwezo wa kiutendaji kwa marais wa vitengo na wakuu wa mashirika, Atabatu Abbasiyya tukufu imekuwa ikiwapa mafunzo mbalimbali watendaji wake kwa ajili ya kuboresha ufanisi wao, asilimia kubwa ya mafunzo wanayo pewa yanahusu kuboresha utendaji wa idara zao.

Kumbuka kuwa lengo la semina hii, ni kuongeza uwezo wa marais na wakuu wa mashirika, wanafundishwa jinsi ya kuwa na mipango ya kimkakati pamoja na usimamiaji wa miradi na utatuzi wa changamoto, wawezeshaji wa semina hii ni wabebozi wa mambo ya utawala, chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: