Ofisi ya turathi nzuri inafanya kazi kubwa kueneza utamaduni wa mapambo ya kuvutia

Maoni katika picha
Ofisi ya turathi nzuri katika idara ya habari na maarifa, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inatilia umuhimu wa kueneza turathi za kiarabu na kiislamu kwa kuangazia fani muhimu ya turathi, ambayo ni fani ya hati za kiaraba na mapambo yanayo wakilisha utamaduni wa kiislamu, aidha fani hiyo inaumuhimu mkubwa katika kueneza maarifa ya Quráni tukufu na Ahlulbait –a.s- kwa kuhuisha fani za waarabu na waislamu, kupitia kuandika herufi kwa uzuri na mapambo sambamba na kuchora matukio ya kihistoria.

Wabunifu wamezingatia upande wa utamaduni kwa kutafiti mazingira yanayo zunguka jamii yetu, na kinacho endana na mazingira hayo kwa kuandika maneno teule, pamoja na picha wanazo chora kwenye mbao, kama sehemu ya kuonyesha fani ya uchoraji wa picha nzuri.

Mtumishi wa idara ya turathi nzuri bwana Muhammad Faalih amesema kuwa: Idara hufanya utafiti na kuibua fani za hati ya kiarabu na mapambo ya kiislamu pamoja na ujenzi wa kiislamu, na kuwa msingi muhimu wa kueneza utamaduni wa Ahlulbait (a.s), tumeandika kwenye mabango fani za kiislamu za aina mbili, tumekamilisha kuweka alama za mapambo kwenye msahafu wa kieletronik wenye ukubwa wa (GB) mradi wa kituo cha maarifa ya Quráni kuifasiri na kuiandika, na kazi ya kuweka mapambo kwenye msahafu wenye ukubwa wa (Rahali) bado inaendelea.

Akaongeza kuwa: Idara ya turathi nzuri ilifanya maonyesho katika mnasaba wa Idi Ghadiir, lakini hayakuzinduliwa kwa sababu ya janga la Korona, wakashiriki kongamano lililoandaliwa na idara ya maonyesho katika mnasaba wa maulidi ya Mtume kwenye eneo la katikati ya haram mbili tukufu, jumla ya mabango mia moja yalishiriki kwenye maonyesho hayo, maandalizi ya kufanya kongamano maalum katika mnasaba wa kuzaliwa mbora wa wanawake wa ulimwenguni, bibi Fatuma Zahara –a.s- yanafanyika, kazi ya kuandika kitabu chenye juzuu tatu kinacho husu ujenzi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi –a.s- inaendelea, na vifaa vilivyo tumika kwenye ujenzi huo, na mapambo ya kiislamu ya mfumo wa mimea na kihandisi, pamoja na kuweka vioo kwenye mauwa, na maandishi ya hati nzuri yanayo pamba haram takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: