Hospitali ya rufaa Alkafeel imeongeza kifaa cha kisasa kwenye maabara yake kinacho fanya kwazi kwa teknolojia ya (PCR)

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imenunua kifaa cha maabara cha kisasa (Abbott Real Time PCR) nacho ni (FDA) kinacho tegemewa na taasisi ya chakula na dawa nchini Marekani, kiongozi wa vifaa vya maabara amesema kuwa kifaa hicho kitasaidia kupima na kugundua vairasi ndogo kabisa katika damu, kwani kinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya (PCR) na kinaweza kuonyesha mambo yafuatayo:

  • 1- Tatizo la ini vairasi aina ya B (Viral Load).
  • 2- Tatizo la ini vairasi aina ya C (Viral Load).
  • 3- Tatizo la ini vairasi aina ya C (Genotyping).
  • 4- Tatizo la ugonjwa wa (TB).
  • 5- Tatizo la upungufu wa kinga ya muili (HIV).
  • 6- Tatizo la (High Risk Human Papilloma Virus).
  • 7- Tatizo la (CMV).
  • 8- Tatizo la (EBV).

Tulifanya utafiti wa kipimo hicho kwa kulinganisha na vipimo vingine ikabainika kuwa, kipimo cha (abbott real time) kinauwezo mkubwa wa kuona virusi vinavyo shambulia ini, hivyo kinatumika kupima wagonjwa wa marahi tuliyotaja na kufuatilia hali zao.

Kwa maelezo zaidi piga simu kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili jioni, kupitia namba zifuatazo: (07602344444) - (07602329999) - (07730622230).
Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora wakati wote kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na vifaa tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa ndani na nje ya Iraq, sehemu kubwa ya huduma zake zinatolewa bure.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: