Kitivo cha famasia katika chuo kikuu cha Alkafeel kimehitimisha semina ya mawasiliano na masoko

Maoni katika picha
Kitivo cha famasia katika chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza semina kuhusu mawasiliano na masoko (Professional communication and selling skills), ambayo imetolewa kwa wanafunzi wa hatua ya nne na ya tano, chini ya ukufunzi wa Ahmadi Kaadhim na Majidi Nabiil iliyodumu kwa muda wa siku nne.

Semina hiyo imefanywa chini ya usimamizi wa idara ya elimu endelevu katika chuo hicho, kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa chuo cha famasia Dokta Saádi Shakuur Walidi Ziyadi amesema: “Kwa ajili ya kuongeza kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa chuo ikiwa pia ni sehemu ya mfululizo wa semina na warsha zinazo tolewa chini ya utaratibu wa chuo, unao lenga kuongeza uwezo wa wanafunzi katika mambo tofauti, sawa iwe katika safari ya masomo ya chuo au baada ya masomo, wanafundishwa masomo muhimu katika sekta ya ubinaadamu na masoko, na sisi kama kawaida yetu tunahakikisha wanafunzi wanafaulu vizuri masomo yaote na wanakuwa tayali kutekeleza wajibu wao”.

Wanafunzi wamesifu semina hiyo na wamesema kuwa inafaida kubwa kwao, wameomba waendelee kupewa semina za aina hii kwani zinaongeza maarifa katika fani wanazo somea na kukuza elimu kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: