Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kinaendelea kutoa dozi ya masomo kwa wanafunzi wake

Maoni katika picha
Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kutoa dozi ya masomo kwa wanafunzi wake wa hatua ya kwanza, kwa ajili ya kufidia masomo yaliyo wapita wakati wa likizo ya Korona, ambapo walikua wanafundishwa masomo ya nadhariyya peke yake kwa njia ya mtandao, masomo wanayopewa hivi sasa yanakamilisha yaliyo pita, ufundishaji wa vitendo humsaidia mwanafunzi kuelewa somo kwa urahisi.

Kiongozi wa chuo Dokta Dhwiyaau Karim Albayati amesema: “Kutokana na maelekezo ya rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali, chuo chetu kinaendelea kutoa masomo chini ya ratiba iliyo pangwa na walimu mahiri, kufidia masomo yaliyo wapita katika msimu wa mwaka jana kutokana na janga la Korona, lililo haribu mfumo wa maisha kwa ujumla ikiwa ni pamoja na mfumo wa ufundishaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: