Mkuu wa hospitali hiyo Dokta Waathiqu Jayadi Hasanawi amesema kuwa: “Baada ya kumaliza miezi nane tangu kufunguliwa kwa kituo cha Alhayaat cha tatu, kilicho jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa, kwa mara ya kwanza kituo kinatangaza kuwa hakina mgonjwa hata mmoja wa virusi vya Korona”.
Tambua kuwa jengo linaukubwa wa mita (1500) na linavyumba (36), vikiwemo vyumba vya idara na dawa, kila chumba kina vifaa vyote vya afya, jengo hilo limekamilisha sifa na vigezo vyote vya afya, kwani lilijengwa rasmi kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.
Kumbuka kuwa jengo la Alhayaat la tatu ni moja ya majengo saba yaliyojengwa na mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, chini ya maelekezo ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kufuatia tamko la Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya katika kupambana na janga hili, na kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa katika hospitali zilizopo. Majengo yaliyo jengwa ni:
- - Majengo mawili katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu katika mkoa mtukufu wa Karbala.
- - Jengo kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu.
- - Jengo katika mkoa wa Baabil kwenye kiwanja cha hospitali ya Marjani.
- - Jengo katika mkoa wa Bagdad kwenye kiwanja cha hospitali ya ibun Qafu chini ya idara ya afya ya Raswafa.
- - Jengo katika mkoa wa Muthanna kwenye kiwanja cha hospitali ya Imamu Hussein (a.s).